July 19, 2021


 KOCHA Mkuu wa Tottenham, Nuno Espirito amesema kuwa nyota wa Real Madrid, Gareth Bale hatarejea ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa 2021/22.

Msimu uliopita Bale alirejea Tottenham kwa mkopo akitokea Klabu ya Real Madrid inayoshiriki La Liga ilikuwa wakati huo timu hiyo inafundishwa na Jose Mourinho.

Awali Bale alikuwa anaweka wazi kwamba anahitaji kurudi katika kikosi chake cha Real Madrid ili aweze kuonyesha makeke yake kwa kuwa alikuwa anaamini kwamba amerudi kwenye ubora wake.

Msimu uliopita ndani ya Ligi Kuu England akiwa Tottenham nyota huyo mwenye miaka 32 alicheza jumla ya mechi 34 na alitupia mabao 16 katika mashindano yote.

Bado mkataba wake ndani ya Real Madrid unaishi ambapo amebakiza mwaka mmoja na pia inaelezwa kuwa kuna ofa nyingine ambazo zipo mkononi mwake hivyo hatakosa timu ya kucheza winga huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic