July 19, 2021


 KLABU ya Horoya leo Julai 18 imetangaza rasmi kusitisha mkataba na mchezaji wao Heritier Makambo.


Kupitia katika ukurasa rasmi wa Horoya ya Guinea wameandika kwamba wanashukuru kwa huduma ya mchezaji huyo ambaye amedumu hapo kwa muda wa misimu miwili.


Nyota huyo aliibuka hapo 2019 akitokea Klabu ya Yanga ambapo alikuwa ni mfungaji namba moja ndani ya Yanga alipotupia mabao 17 na kuwa namba tatu kwa washambuliaji wenye mabao mengi.

Namba moja alikuwa ni Meddie Kagere ambaye alitupia mabao 23 na alisepa na kiatu cha ufungaji bora.


Huenda dili lake la kurudi Yanga likajibu kwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi hao ambao wamemaliza ligi wakiwa nafasi ya pili.

Hivyo kuangwa kwake rasmi na mabosi wake hao kunafanya dili lake kuwa jepesi kuweza kutua Yanga.


9 COMMENTS:

  1. Huyo hafai Yanga hii kama hata huko Horoya katemwa.

    ReplyDelete
  2. Timu ya wakongo hahaha

    ReplyDelete
  3. Timu ya wakongo hahaha

    ReplyDelete
  4. Kama katemwa huko horoya,, yanga ndio ataperform, yanga Sasa inahitaji mabadiliko ya kweli ili klabu iweze kusonga mbele

    ReplyDelete
  5. Mbona hata Morison alitemwa huko alikotoka, suala la mkataba kuisha, huwezijua mazungumzo yao mpaka wasimuongezeee mkataba

    ReplyDelete
  6. Karbu sana makambo young bado tunakuhitaji

    ReplyDelete
  7. Sababu ya kutopata nafasi ya kucheza ni kuwa kapoteza kiwango hivo katemwa na yanga imeambulia matapishi

    ReplyDelete
  8. Striker yupi mlisajili kwa kuvunja mkataba.... Tuanzie hapo kwanza. Mlipiga kelele nyingi kuwa mnamsajili lkn wapi mpaka jamaa wameamua kusitisha mkataba, nadhani sasa ndo mnaweza kumsajili

    ReplyDelete
  9. Hata kama kaachwa lakini bado anaweza kutusaidia hivyo viongozi kama kuna uwezekano aje atatusaidia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic