July 20, 2021


 IMEELEZWA kuwa mabosi wa Simba wapo kwenye mazungumzo ya mwisho kukamilisha dili la mshambuliaji wa Mbeya City, Kibu Denis.

Mshambuliaji huyo alikuwa anatajwa pia kuwa kwenye rada za Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi na ilikuwa inatajwa kuwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la nyota huyo.

Ndani ya Mbeya City nyota huyo ametupia abao 7 na ametoa pasi tatu za mabao hivyo akikamilisha dili lake la kujiunga na Simba ana kazi ya kupambana kupenya kikosi cha kwanza kwa kuwa atakutana na washambuliaji wenye ushkaji mkubwa na nyavu.

Uwepo wa John Bocco mwenye mabao 16, Meddie Kagere mwenye mabao 13 na Chris Mugalu mwenye mabao 15 kutamfanya awe na kazi ya kuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Didier Gomes.

 Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara aliweka wazi kwamba wamekamilisha usajili wa nyota watatu ambao watatambulishwa hivi karibuni.

3 COMMENTS:

  1. Wapi Ilanfya naye alikuwa kwenye Rada za YANGA,,,,,Thiiiiimba

    ReplyDelete
  2. Kusajili kwa mihemko hapa bongo kutaisha lini! Yani mpira wa TANZANIA ni mavi tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic