July 20, 2021


 MZEE wa kukera ndani ya uwanja, Bernard Morrison kwa sasa amesharejaea ndani ya ardhi ya Tanzania baada ya kutokuwepo kwa muda kutokana na matatizo ya kifamilia.

Nyota huyo ambaye mabosi wa Azam FC hawana hamu naye kutokana na kitendo chake cha kuanzisha faulo harakahara kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ulikuwa ni nusu fainali huenda atakuwa kwenye kikosi kitakachoivaa Yanga.

Pia kipa namba moja wa Namungo FC, Jonathan Nahimana naye hana hamu naye kwa kuwa alimtungua bao akiwa nje ya 18 kwenye mchezo wa ligi jambo ambalo liliwafanya mabosi wa Namungo kuyeyusha pointi tatu mazima kwa kufungwa mabao 3-1.

Mtu wa karibu wa Morrison amesema kuwa nyota huyo tayari amerudi Dar tayari kwa ajili ya mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga.

"Tayari Morrison yupo Dar na hivyo anaweza kuwa kwenye kikosi kitakachoanza dhidi ya Yanga ikiwa mwalimu atahitaji," ilieleza taarifa hiyo.

Hivi karibuni, Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola aliweka wazi kwamba Morrison atarejea kikosini hivi karibuni.

"Morrison atarejea kikosini hivi karibuni kwa kuwa alikuwa kwenye matatizo ya kifamilia, alikuwa kwao nchini Ghana," .

Kwenye mchezo wa ligi wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa, Julai 3 ukisoma Simba 0-1 Yanga aliyeyusha dk 90.

Wanatarajiwa kukutana tena Kigoma, Julai 25 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.

7 COMMENTS:

  1. Ndiye anajirusha kuomba Penati????fungeni Goli likataliwe utasikia oh kashika,oh tunataka hiyo Birihani mbele ya Wananchi Kama hamtarishwa Ugali wa Mtama na Kitimoto

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shabiki maandazi, shabiki oya oya hana anachojua

      Delete
  2. Safari hii waamuzi kuweni makini muone kitakachotokea

    ReplyDelete
  3. Mwambieni achezeshe manara na kaburu maana nyinyi mkifungwa hamkosi visingizio

    ReplyDelete
  4. Kwni katkea wpi mpaka Wana simbilis wanamuona yye malaika wao kama coo jangwan

    ReplyDelete
  5. Simba hawana geni mambo yao yoote kutoka ktk mechi za kombe la mabingwa mchezo wao haujabadilika unatambulika,mabao yao ni cross za v,kona kwa boko au mkenya na hutegemea penalt za kujiangusha Morison ndani y 18 hawana jipya hii safari simba 0 yanga 1.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic