MUDATHIR Yahya, kiungo wa Azam FC amefunga bao la kufunga msimu wa 2020/21 kwa timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.
Inakuwa ni rekodi yake ndani ya Azam FC kwa msimu wa 2020/21 ambao walikuwa wanapambana kutimiza jambo lao lililokwamwa.
Bao hilo alipachika mbele ya Ruvu Shooting jana Julai 18 Uwanja wa Mabatini kwa pasi ya Idd Seleman, 'Nado'.
Ushindi huo unaifanya Azam FC kukamilisha msimu wa 2020/21 ikiwa nafasi ya 3 na pointi zake ni 68 baada ya kucheza mechi 34.
Mabingwa wa ligi ni Simba ambapo wamekusanya pointi 83 baada ya kucheza jumla ya mechi 34.
Aliyefungua ukurasa wa mabao ndani ya Azam FC alikuwa ni Prince Dube ambaye ametupia jumla ya mabao 14 ilikuwa ni bao moja mbele ya Polisi Tanzania.
0 COMMENTS:
Post a Comment