July 20, 2021

 


WANASUBIRIWA Fiston Mayele na Heritier Makambo pekee ili Yanga kukamilisha idadi ya wachezaji watano kutoka DR Congo ambao wapo kwa kazi maalum ambayo ni kuirudisha Yanga katika makali yake pamoja na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.

 

Yanga msimu ujao wanatarajiwa kushiriki katika michuano ya kimataifa mara baada ya Tanzania kupata tiketi ya kuingiza timu nne katika michuano hiyo huku Yanga ikishika nafasi ya pili katika ligi kuu msimu huu.

 

Yanga chini ya mwenyekiti msaidizi wa kamati ya usajili ya timu hiyo, Injia Hersi Said alisema kuwa “Kuelekea katika msimu ujao ambao tutashiriki michuano ya kimataifa lazima tutafanya usajili ambao utatufanya tuwe na timu bora ya ushindani na si ushiriki,”alisema kiongozi huyo.

 


Yanga msimu huu imemaliza ligi ikiwa ina wachezaji wawili wa Kikongo ambao ni Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe ambao walisajiliwa katika usajili uliopita wa dirisha kubwa la usajili wakitokea katika klabu ya AS Vita ambapo kabla ya ujio wao alikuwepo Papy Tshishimbi ambaye alikuwa ni Mcongo pia.

 

Tayari msimu huu Yanga imeshakamilisha usajili wa mkongo mwingine kutoka katika klabu ya AS Vita, Shabani Djuma anayecheza katika eneo la beki wa kulia na kufanya idadi kamili kuwa Yanga inamiliki Wakongo watatu katika kikosi chake.

 

Yanga kwa sasa inahusishwa na usajili wa mshambuliaji wa AS Vita ya nchini DR Congo, Fiston Mayele na mshambuliaji wa Horoya FC, Heriter Makambo ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji wa Yanga.

 

Makambo licha ya kucheza katika klabu hiyo ya Horoya iliyopo nchini Guinea, mshambuliaji huyo ana uraia wa DR Congo na kwa sasa yupo huru baada ya mabosi wake kufikia makubaliano ya kuachana naye.


Hivyo kama Yanga itakamilisha usajili wa washambuliaji hao wawili itakamilisha idadi ya wachezaji watano wenye uraia wa Congo ambao ni Mukoko Tonombe,Tuisila Kisinda, Shabani Djuma,Fiston Mayele na Heritier Makambo.

7 COMMENTS:

  1. Sidhani kama ni jambi jema kujaza karibu nusu ya first eleven kutoka nchi moja, wakifeli unakosa option ma vionjo toka mchi zingine. Tujifunze toka wolves

    ReplyDelete
  2. Pendekeza aletwe yupi kutoka nchi gani

    ReplyDelete
  3. Tunajenga Congo FC baada ya Burundi FC kufeli

    ReplyDelete
  4. Ac Vita B ya Bongo hahaha

    ReplyDelete
  5. Wakongo bei yao iko chini wananunulika ndo maana tunawajaza hapa kwetu Yanga.

    ReplyDelete
  6. Yan hakuna kitu kuzur kumpiga mtani wako alaf bado akapata nafac yakuxbuli mechi nyine Tena nahyo nyingine akifungwa ataxbili nyingine lahaaaaaah ilioje jaman waoooooh mtu kalamba nyasi feisalu fei Toto zizu staili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic