July 21, 2021

JULAI 29, mwaka 2019 kutoka katika kinywa cha msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara yalitamkwa maneno yafuatao: “Tukio letu la wiki ya Simba limeigwa maeneo mbalimbali, lakini sisi tutataka kulifanya kwa ubora zaidi, na kauli mbiu yetu itaitwa 'Iga Ufe, this is Next Level.”

Hii ilikuwa ni katika maandalizi ya tamasha lao kubwa la Simba Day.

Hapa Manara alitaka kuonyesha kuwa kuna utofauti wa wazi na mkubwa uliopo kati ya klabu ya Simba na klabu nyingine hasa za Ligi Kuu Bara. Kwangu hii ni moja kati ya kauli mbiu ‘Slogan’ bora zaidi ambazo zimewahi kutolewa na Manara kuihusu Simba.

Katika miaka ya hivi karibuni ni kweli Simba wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuiweka kauli mbiu hii katika utekelezaji, na ndiyo maana leo hii tunaizungumzia klabu ambayo imefanikiwa kutawala soka la Tanzania kwa kutwaa ubingwa kwa misimu minne mfululizo.

Simba wanastahili pongezi kwa mafanikio haya makubwa kwani mpaka sasa imepita miaka 41 tangu mara ya mwisho klabu moja kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa angalau misimu minne mfululizo.

Mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa mwaka 1980, ambapo Simba walitwaa ubingwa kwa misimu mitano mfululizo.

Lakini Simba pia wameonyesha ukuaji mkubwa katika uthubutu wa kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa ambapo ndani ya misimu mitatu, wamefanikiwa kufika katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili.

Mafanikio haya makubwa ya Simba uwanjani, bila shaka yamechagizwa sana na usajili wa wachezaji bora ambao wengi wamefanikiwa kufikia matarajio ya viongozi waliowasajili.

Simba hawajatawala soka la uwanjani pekee bali hata katika mitandao ya kijamii ambapo mwishoni mwa mwaka jana, kwa mujibu wa mtandao wa Transfer Market unaoaminika kwa kuelezea takwimu za soka, uliutaja ukurasa wa soka wa Simba kwenye akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa ukurasa namba moja kwa ukuaji miongoni kurasa za klabu duniani.

Kupitia mafanikio ambayo Simba imeyapata, ni wazi klabu nyingine za Tanzania zimepata nafasi ya kujifunza, jambo ambalo linazidi kuamsha ari ya kupambana na kufanya mabadiliko muhimu ya uendeshaji wa klabu hizo ili kufanya vizuri zaidi.

Lakini licha ya mafanikio hayo makubwa ya Simba, bado kuna baadhi ya changamoto za ‘kiujanjaujanja’ wa baadhi ya viongozi wa klabu hiyo, ambao unaonekana kutaka kutia doa jitihada za makusudi zinazofanywa kufikia malengo yao ya kuwa miongoni mwa klabu bora Afrika na duniani kwa ujumla.

Kwanini nazungumza hili? Hivi karibuni gumzo kubwa lilikuwa ni sauti ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Dokta. Arnold Kashembe ambaye kupitia kituo kimoja cha habari alisikika akizungumzia makosa makubwa yaliyofanywa na viongozi wa juu wa klabu hiyo katika maamuzi ya mambo nyeti.

Kwa mujibu wa Kashembe kumekuwa na madudu makubwa yaliyofanyika kwenye baadhi ya maeneo kama vile; mikataba ya haki za matangazo ya televisheni, ubinafsi wa baadhi ya viongozi wanaotaka kuitumia klabu hiyo kwa faida zao, na hata ishu ya mabadiliko ya uendeshaji wa klabu.

Ukimya wa uongozi wa Simba baada ya shutuma hizi unaleta taswira mbili kubwa moja shutuma hizi ni za ukweli, na hakuna namna ya kutumia nguvu kuzipinga.

Au mbili shutuma hizi si za kweli na labda klabu imeona hakuna haja ya kutumia nguvu kubwa kushindana nazo wakati wana kazi kubwa ya kutimiza malengo yao ya kushinda kombe la Shirikisho kwenye fainali dhidi ya Yanga, baada ya kutetea ndoo ya Ligi Kuu Bara.

Katika hili nadhani tuache wakati utatupa majibu sahihi ya kipi ni pumba na lipi ni la ukweli, lakini nadhani kama klabu ambayo ina malengo ya kufikia daraja A la klabu bora za Afrika, na labda duniani ni lazima wahakikishe wanahusianisha malengo yaliyo kwenye mipango ya karatasi na uhalisia wa mabadiliko yanayohitajika.

Ni lazima wakubali kutoa sadaka kubwa ya kuachana na baadhi ya watu, ambao wanaonekana kuwa kikwazo katika mpango huo wa mafanikio.

 

11 COMMENTS:

  1. Umesema wamefanikiwa uwanjani sababu ya usajili mzuri, ungetumia muda huo pia kuwakumbusha vilaza wanaodhani corona, uchawi na kubebwa ndo vinaleta mafanikio ili nao wawekeze kwenye timu la sivyo wataendelea kukodoa mimacho tu huku wenzao wakiendelea kufanya vizuri

    ReplyDelete
    Replies
    1. Upumbavu mtupu huwezi kuanika gazeti zima hapa la kuizodoa simba Timu yenye mafanikio na kuubeba mpira wa nchi kwenye next level kwenye kuingiza timu nne kutoka Tanzania kushiriki kimataifa,kuanzisha mchakato wa uendeshaji wa timu zetu kisasa,kuanzisha matamasha ya kuhamasisha wanachama mashabiki na wapenzi,Klabu ya Kwanza kabisa kutoka Tanzania na ukanda wa Africa ya mashariki kuendeshwa na CEO Mwanamama,klabu pekee east Africa kukaa kwenye nane Bora ya Africa ndani ya miaka mitatu.klabu pekee Tanzania kwa sasa yenye ustahamilivu wa kukaa na wachezaji na makocha
      kwa muda mrefu na mengi mazuri ya simba tunaweza kuelezea tusifike kikomo lakini haya yote mzuri ya simba wapumbavu hawayaoni jinsi ya kuyaelezea kwa upana wake isipokuwa wanatafuta negative making up story na kuzifanya ndio habari.Sasa Kama Simba ndio Mwenyekiti wake wa timu Bwana Mangungu angemwambia Manula umeuza mechi Kama alivyofanya mwenyekiti wa Yanga hali ingekuwaje kwa waandishi juu ya simba? Au simba ingetimua makocha wanne ndani ya msimu mmoja wa ligi story zingekuwaje juu ya simba. Au simba ingekuwa inadilisha karibu wachezaji wote kila msimu Kama wanavyofanya Watani wao hali ingekuwaje kwa waandishi? Na vipi Kama simba wangekuwa ina wachezaji wao wa zamani na wa Sasa bado wanamlilia haki zao kutolipwa Kama akina yondani,tambwe,Dantena wachezaji kadhaa wanaosotea haki zao yanga hali ingekuwaje?.kama ujanja ujanja basi huu wa Yanga ni ujambazi. Hawa wanaoidai Yanga Kama ingekuwa simba ingekuwaje? Huwezi kuelezea machache mapungufu ya kubuni kwa ukubwa usiokikomo halafu ukanyamaza kimya kushindwa kuyaelezea mengi mazuri ya taasisi fulani halafu eti unajifanya unania ya kujenga? Ni unafiki na uchawi kwa bahati mbaya ujinga huu unachapishwa hapa kwenye mtandao unaojipiga kifua eti wapo kwa ajili ya kujenga mpira wa watanzania.Kweli?

      Delete
  2. Naona mwandishi unaleta chokochoko ili ututoe mchezoni.
    Umetumwa?!!!!!

    ReplyDelete
  3. Bumbuli atatuhabarisha jambo letu!

    ReplyDelete
  4. What is your intention ndugu mwandishi, usitumie kalamu yako kugombanisha watu ili timu nyingine update upenyo walipita,hahaha wanasimba tuwe Makini tuwekitunkimoja msimu mpya unaanza tusikubali kurubumiwa ilituweze kupata back 2 back kumi.simba nguvu moja.

    ReplyDelete
  5. Daah prexha ya nni Kwan Tim c inaendesha nawataalam wasoka walio bobea mda unaruhusu tutaona tu mcpate tabu yakuwachukia waandixhi hiyo ndo kaziyao mlitka wandike Mambo gan sas mapenz au

    ReplyDelete
  6. kichwa cha habari kilitakiwa kiwe sauti ya xxx yasikika akilalamikia xxx ila unapoiongelea taasisi ulipaswa kuweka mizania ili kujua undani na mashiko ya jambo lenyewe. lakini hapo kiini cha habari hakiendani na namna ulivyoianza hiyo habari. kwa sababu unachookiita ujanjaujanja haujaonyesha namna unavyoathiri hayo mafanikio uliyoyataja mwanzo.

    ReplyDelete
  7. Kitenge na Kashembe ni ........... wanajulikana sasa Saleh na wewe jadili vitu vya maana. Je Azam ushawauliza juu ya hilo?
    Je Ushaanza kuoperate?

    Vitu vingine haviitaji form 4 ya kureset

    ReplyDelete
  8. Upigaji hela lazima uendelee na kuwaacha wale wanaojiita mashabiki nguli mara kindakindaki wakiendelea kunuka jasho na vikwapa, hiyo ndo FOOTBALL ya TANZANIA

    ReplyDelete
  9. HATA FLORENTINO PEREZ NAE NI MJANJA MJANJA. AU NAKOSEA?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic