MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji, 'Mo' ni miongoni mwa waliohudhuria mchezo wa leo Uwanja wa Mkapa.
Simba inacheza na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo Simba itakabidhiwa taji la ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Simba kukabidhiwa taji la ligi mbele ya Namungo FC ya Lindi.
Ikumbukwe kwamba msimu uliopita wa 2019/20 ni Namumgo ilicheza na Simba wakati timu hiyo ikikabidhiwa taji hilo.
Katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, dk 90 zilikamilika na ubao ukasoma Namungo 0-0 Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment