HAJI Manara ingizo jipya ndani ya Yanga akiwa kwenye kitengo cha habari amesema kuwa watafunika kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi, kesho Uwanja wa Mkapa huku akiwasifu viongozi wa Yanga kufanya kazi kwa ushirikiano.
Kesho inatarajiwa kuwa ni kelele cha Wiki ya Mwananchi ambapo kulikuwa na matukio mbalimbali yakifanywa kabla ya siku ya mwisho. Matukio ambayo yalikuwa yanafanyika ilikuwa ni pamoja na kujitolea damu, kufanya usafi pamoja na matendo ya huruma kwa jamii.
Manara ambaye alikuwa Ofisa Habari wa Simba kwa muda wa miaka sita sasa anahudumu ndani ya Yanga huku akibainisha kuwa yeye ni kama mchezaji vile kuhama timu moja hakuna tatizo.
Kuhusu tukio la kesho Manara alisema:”Ukiacha tukio la mimi kuingia na msanii kwa helkopta kubwa ya kisasa kulikuwa na jambo gani ambalo sisi, (Simba) tuliwazidi Yanga kwa ukubwa wa tamasha? Tuliweka maskrini yetu upande wa pili yalidoda waliingia watu 20.
“Mwaka jana sisi Yanga hatukuwaweza lakini kwa sababu ya ubishi wangu na kujitutumua tukaonekana tupo sawa. Kwa wiki ambayo nipo Yanga, Yanga wanafanya kazi kama taasisi, unakaa unaona namna management, (utawala) inavyofanya kazi.
“Tofauti na sisi ni one man show team, (timu ya mtu mmoja) kwamba mtu mmoja anapanga kila kitu, huku wenzentu hawa nimeungana nao wanafanya kazi kama taasisi hawa hawafanyi kazi kama timu ya mtu mmoja. Ndio maana unaona wakipanga mambo yao yanakwenda sawa.
“Mungu hakuwa amewajalia kuwapa trophies, (ubingwa) ilikuwa ni suala la muda tu kwa sababu usajili waliofanya msimu huu mimi umenifanya pia nijiunge nao. Kwa namna ambavyo wamefanya. Sasa wanakwenda kuchukua mataji yao kwa sababu wanayo 27, wanakwenda kushinda mataji. Mwezi wa tano ligi itakapokuwa inamalizika Yanga watakuwa mbali sana,” amesema Manara.
Kama kila kitu walichopanga kilikwenda sawa ina maana mautumbo yote yale ya msimu uliopita yalikwepo kwenye mipango yao, Kama ndo hivyo bac hakuna kitu hapo na kuhusu trophies msahau labda tophies
ReplyDeleteAnajikamua kuonesha kuwa yeye ni mkubwa kuliko Yanga 😃
ReplyDeleteNdio washamfanya hivyo wasije wakasema anawahujumu baadaye hawachelewi utopolo
DeleteNdo maana nugaz kamuita msukule
ReplyDelete