August 29, 2021


 KIPA namba moja wa KMC, Juma Kaseja amesema kuwa uchawi wake mkubwa ni mazoezi jambo ambalo linamfanya kuwa bora muda wote awapo uwanjani.


Nyota huyo kwa msimu wa 2020/21 aliweza kukosekana kwenye mechi 6 za Ligi Kuu Bara kati ya 34 na KMC ilimaliza ikiwa nafasi ya 5 na pointi zake 48.

Kaseja uwezo wake ni mkubwa kwenye mikono yake na ni miongoni mwa makipa wenye uzoefu ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa amezitumikia timu zote mbili kubwa ile ya Simba na Yanga pia kwa nyakati tofauti.

Kaseja amesema:”Uchawi wangu mimi ni mazoezi, unaona kabisa wengine wakiwa wamepumzika mimi nafanya mazoezi tena kwenye jua kali. Hilo tu kwani ili uweze kuwa vizuri uwanjani ni lazima ufanye mazoezi na kufuata program ambazo unapewa.


“Kwa msimu ujao malengo makubwa ni kuona kwamba tunatimiza yale malengo ya timu kisha hapo itafuata malengo binafsi kitu cha kwanza ambacho tunakipa kipaumbele ni malengo ya timu,” alisema Kaseja.


Kwa sasa timu ya KMC imeweka kambi Morogoro ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya 2021/22.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic