August 29, 2021


THOMAS Tuchel, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa bado hajafurahishwa na kitendo cha mchezaji wake kuonyesha kadi nyekundu mapema kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Ni beki wake Reece James ambaye aliweza kuonyeshwa kadi nyekundu dk 45 kwa kucheza faulo iliyosababisha penalti baada ya mwamuzi kuamua iwe hivyo na ikafungwa na Mohamed Salah dk 45.

Bao la nyota huyo raia wa Misri Uwanja wa Anfield liliweza kuwafanya Liverpool kusawazisha bao la Kai Havertz aliyepachika dk 22.

Tuchel amesema:"Sijapenda kabisa ile kadi nyekundu ya mapema ambayo mchezaji wangu alionyeshwa na sio namna ambavyo tumecheza tu na Liverpool bali kiujumla ilikuwa kama tumetekwa nyara.

"Hali halisi kiujumla ilinifanya nishindwe kuelewa maamuzi ambayo yalifanyika. Sijasema kwamba maamuzi hayakuwa sahihi hapana, lakini sijapenda namna ambavyo mwamuzi aliweza kuangalia picha pekee," .


2 COMMENTS:

  1. Uandishi gani huu, raia wa misri hana jina,

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kukurupuka wewe!!! Umesoma vizuri hiyo habari? Mwandishi keshamtaja jina kwenye aya (paragraph)ya pili halafu akaendelea kumuelezea zaidi kwenye aya ya tatu lakini wewe unajifanya upo smart kumbe unajionesha ni jinsi gani ulivyokuwa mtupu kichwani

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic