August 28, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa utawaita wachezaji wote wa timu hiyo ambao wapo kambini kwa sasa kwenye timu ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia kuja kuhudhuria katika kilele cha Wiki ya Mwananchi.


Timu ya Taifa ya Tanzania 
iliingia kambini Agosti 25, tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo dhidi ya DR Congo utakaofanyika Septemba 2, nchini DR Congo.


Wachezaji Yanga ambao wameenda kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania ni Feisal Salum, Dickson Job, Zawadi Mauya na Ramadhani Kabwili.

 

 Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabit Kandoro, alisema kuwa tayari wameshawasiliana na uongozi wa timu ya taifa juu ya kuwaomba wachezaji hao kwa ajili ya kuja kushiriki Siku ya Mwananchi kisha kurejea tena kambini.


“Tayari tumeshaongea na uongozi wa timu ya taifa ya Tanzania juu ya kuwaomba wachezaji wetu wote katika mchezo wa kilele cha siku ya Mwananchi dhidi ya Zanaco FC na tayari ombi letu limekubaliwa.

 

“Hivyo mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi juu ya kuwakosa wachezaji hao na kilichobaki kwa sasa mashabiki wanatakiwa wafike kwa wingi kwani kutakuwa na mambo mengi mazuri kwa ajili yao,” alisema kiongozi huyo.

3 COMMENTS:

  1. Tunawaombea mazr na ushnd mzur Taifa stars

    ReplyDelete
  2. Hata muwaite mtapigwa tu maana timu bovu hilo.... Andaeni visingizio

    ReplyDelete
    Replies
    1. Walah,, leo zanaco hatowaacha salama lazma walie

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic