September 22, 2021


MWANDISHI mkongwe kwenye masuala ya Habari za Michezo, Tanzania mwenye rekodi za kufanya kazi mbalimbali kubwa ndani na nje ya Tanzania, Saleh Jembe amesema kuwa kuna haja ya kuupa thamani mpira wa Tanzania kwa kuanzia na suala la viingilio.


Maneno hayo amaeyazungumza kwenye kipindi cha Krosi Dongo ambacho kinarushwa ndani ya 255 Global Radio pamoja na Global TV Online.

Jembe amesema:"Ikiwa sehemu kuna msanii anatumbuiza labda ni Kiba, (Alikiba) au Diamond kiingilio ni shilingi elfu ishirini ama elfu 50 watu wanakwenda.

"Lakini unakwenda kuwaona wachezaji kama akina Morrison,(Bernard) Banda, (Peter) Makambo,(Heritier) Aucho,(Khalid) Djuma na burudani ya uwanjani unaijua jinsi ilivyo ni raha kuna vitu vingi.

"Unakutana na watu tofauti lakini shilingi elfu 10 unaona kama unaonewa, si kweli sisemei hii mifano unaweza kukataa hapana, nimepata bahati ya kwenda Ulaya nimeona namna jinsi ilivyo huko.

"Tiketi ya kiwango cha chini nililipia shilingi laki moja na ishirini na tano na mara ya mwisho niliwahi kulipa tiketi kwa shilingi laki tatu na themanini ya Tanzania achana na gharama ya tiketi ya ndege.

"Sio kwamba mimi ni tajiri hapana ni ile furaha yangu ya kwenye mpira, nakumbuka namna nilivyokuwa Uwanja wa Anfield watu wanaimba najiskia raha nimetumia fedha lakini ile furaha bado nipo nayo.

"Tunapaswa kuupa thamani mpira wetu, thamani yake ni kubwa tena kwa mechi za Simba v Yanga hii ni lazima iwe ya thamani. Kuna marafiki wengi wakubwa kutoka nje walikuwa wanakuja kuutazama mchezo hivyo kuna haja ya kuipa thamani," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Tunapaswa pia kuwapa thamani wachezaji wazawa Kama akina John Bocco, Fei toto, kapombbe, mudathir, na wengineo tusiangalie tu wageni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Thamani ya wachezaji wazawa ipo kwenye uwezo wao uwanjani sio kuvimbishwa kichwa kijinga. Simba inawathaminisha Sana wachezaji wazawa Kuna uelewa mkubwa ndani ya Simba. Najua kama Kagere angekuwa Mzawa watu wangeapiza Sana kwa kutokupewa Muda wa kutosha uwanjani lakini ndani ya Simba ushindani wa namba ni mkubwa na wachezaji waliojua raha ya ushindani wa namba ndani ya Simba leo wameshaondoka kwenda kwenye ushindani wa namba zaidi ndani ya Alhaly ya Misri na kadhalika na Wachezaji wetu wanapaswa kuwa na wivu pia wakwenda kwenye neema zaidi.

      Delete
  2. Acha zako,wananchi wenye vipato vya chini wasiende mpirani?

    ReplyDelete
  3. Wazawa wajitume cyo wakina Banda,Kibabage au Adam Adam wanarudi nchini na visingizio lukuki,wajitume ili watusue kimataifa kama Luis,Chama,Msuva au Samata

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic