IMETHIBITISHWA kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Balama Mapinduzi tayari amekamilisha programu maalum za mazoezi binafsi ambazo alipewa na benchi la ufundi na kujiunga na wenzake, hivyo hatima yake ndani ya kikosi cha Yanga ipo chini ya kocha mkuu wa timu hiyo Nasreddine Nabi.
Balama alipata jeraha la enka katika mazoezi ya kikosi cha Yanga kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda mwezi Juni mwaka jana, na kufanyiwa upasuaji mara mbili hivyo kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya mwaka sasa.
Daktari wa Klabu ya Yanga, Shecky Mngazija alisema: “Kwa sasa Balama Mapinduzi tayari amemaliza programu binafsi za mazoezi maalum aliyokuwa amepewa na benchi la ufundi na ameanza kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake.
“Hivyo kutokuonekana kwake hakuna mahusiano na majeraha bali ni maamuzi ya kocha mkuu ambaye kutokana na utayari wa mchezaji husika anaweza kumpa nafasi.”
Pole sana kijana, ila asiwe na haraka ya kuanza na mechi tough, aanze na zile nyepesi.
ReplyDeleteMechi kubwa hii inahitaji walio timamu kwa kiasi kikubwa, binafsi sihauri acheze labda tukiongoza 4-0 bila ndo aingie
ReplyDeleteLabda mkicheza na Mwanakarenge Fc ya Bagamoyo
DeleteTukicheza na hawa hawa makoro fc!
DeleteMnaweza kuwaita watu makolo bila kujua maana yake kumbe nyie wenyewe ndo makolo
DeleteKocha mwenye akili timamu hawezi kumchezesha
ReplyDeleteLabda kocha apangiwe kikosi
ReplyDelete