September 28, 2021

 


FT:Biashara United 0-0 Simba

Biashara United ya Mara wanapenda kujiita Wanajeshi wa Mpakani wamegawana pointi mojamoja na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara.

Dakika ya 90 Bocco anakosa penalti baada ya kipa wa Biashara United kuokoa hatari hiyo.

Dakika ya 82 Manula anaokoa hatari ya faulo iliyopigwa na Salum.

Dakika ya 80 Manula anaokoa hatari langoni mwake.

Dakika ya 76 Nyoni anafanya jaribio linaokolewa na James.

Dakika ya 74 Banda anapiga shuti linakwenda nje ya lango.

Dakika ya 72 nyota wa Biashara United anapewa huduma ya kwanza.

Dakika ya 68 Nyoni anakosa nafasi ya kufunga.

Dakika ya 61 Nyoni anapeleka mashambulizi Biashara United.

Dakika ya 58 Mhilu anaingia anatoka Dilunga,  Peter Banda anaingia anatoka Inonga

Dakika ya 49 James anaokoa hatari, Duncan Nyoni anaingia anatoka Bwalya, anaingia Zimbwe anatoka Kapombe

Dakika ya 46 Kennedy Juma anapewa huduma ya kwanza, Nzingha anaingia kuchukua nafasi ya Zuber wa Biashara United 




Kipindi cha pili kimeanza 

UWANJA wa Karume 


LIGI KUU BARA 

Mapumziko 

Biashara United 0-0 Simba

Dakika 45 zinakamilika,  Zinaongezwa 4

Biashara United 0-0 Simba

Dakika ya 44 Mpapi anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Dilunga 

Dakika ya 41 Mwenda anapiga shuti linaokolewa na James 

Dakika ya 40 Manula anaokoa hatari 

Dakika ya 36, Bwalya anapiga kona haileti matunda na Kagere anakosa nafasi ya kufunga

Dakika ya 33 Kagere anakosa nafasi ya wazi pia nyota wa Biashara United Denis anakosa nafasi ya wazi ndani ya 18 baada ya kupaisha mpira

Dakika ya 29 Bwalya anapiga kona haileti matunda kwa Simba, Biashara United wanaanua majalo

Dakika ya 28, Omary Rashid wa Biashara United anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Inonga.

Dakika ya 26 Israel Mwenda anafanya jaribio akiwa nje ya 18 linaokolewa na James. 

Dakika ya 21 Bwalya anajaza majalo yanakutana na mikono ya kipa James.

Dakika ya 20 Bwalya anapiga kona ya kwanza haileti matunda,  Kagere anafanya jaribio la kwanza kwa kichwa linakwenda nje ya lango. 

Dakika ya 16 Kenedy anamchezea faulo kipa wa Biashara United.

Dakika ya 13, Bocco anacheza faulo kwa mchezaji wa Biashara United.

Dakika ya 12 Kenedy Juma anarejesha mpira kwa Manula anachezewa faulo 

Dakika ya 11 Mangalo anaanua majalo.

Dakika ya 9 Biashara United wanapata faulo Uwanja wa Karume Mara nje ya 18.

Dakika ya 6 Kapombe anapeleka mashambulizi Biashara United.

Dakika ya 4 Redondo anachezewa faulo.

Dakika ya 3 Kapombe anaanua majalo baada ya Kennedy Juma kujichanganya.

Dakika ya 2 Dilunga anachezewa faulo

6 COMMENTS:

  1. Hahaha ww subili watakalia ty km juzi

    ReplyDelete
  2. Kama kuna wachezaji watulivu kwenye upogaji wa penalt si ndani ya bali TANZANIA basi ni Erasto Nyoni sasa kiherehere Cha nini jamani Boko? Mchezaji mwenye historia inayoumiza ndani ya Simba katika upigaji wa penalt. Simba tuna Tatizo la fowadi hawa akina Boko hivi sasa watateseka Sana kwa sababu akina Chama walikuwa wakiwafichia ubovu wao.piga ua Simba wanatakiwa kumuamimi na kumuaminisha Sakho kama fowadi namba moja naimani safu ya ushambuliaji ya Simba itakuwa kwenye mikono ya ushindi chini ya Sakho achana na hawa shikamoo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Boko penati zote muhimu huwa anakosa kuanzia na Mazembe, Ruvu msimu uliopita ila anapenda kulazimisha ili awe mfungaji bora baadae utasikia tunaomba radhi

      Delete
  3. Team yangu ya Simba inabidi mwalimu abadili mbinu za uchezaji,kwa mpira ambao Simba amecheza match tatu zilizopita nahisi hata club bingwa hatutafika mbali,Simba hajawahi kucheza match tatu mfululizo asipate at least goal moja

    ReplyDelete
  4. Nilisema mimi. Ni wakati sasa Da Rosa awaamini vijana. Hali halisi imeonekana leo Karume, Musoma. Amiwapanga Sakho, Muhilu, Kibu, Nyoni Dancan, Abdulswamadu na wengineo hakika kitaeleweka

    ReplyDelete
  5. Mbona mapema sana,yaani mechi ya kwanza tu mbinja nyiingiiiiii

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic