KLABU ya KMC imeanza kwa kuangusha pointi tatu kwenye mchezo wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22.
Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Karatu na ulikamilika kwa ubao kusoma Polisi Tanzania 2-0 KMC.
Mabao yote ya Polisi Tanzania yalifungwa na Vitalis Mayanga mshambuliaji wa Polisi Tanzania ilikuwa ni dakika ya 3 na lile la pili dakika ya 30.
Kipa namba moja wa KMC, Juma Kaseja hakuwa na chaguo la kufanya zaidi ya kuokota michomo hiyo miwili kwenye milingoti yake.
Ni kipindi cha kwanza mabao yote yalipachikwa kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.
Mikono ya Metacha Mnata imeanza bila kuokota mpira katika wavu wake dakika zote 90 huku nyota wale wa KMC, Miraj Athuman, Awesu Awesu wakiwa ni miongoni mwa nyota waliocheza leo wakiwa na uzi wa KMC.
GOLI LA PILI LIMEFUNGWA DK YA 19
ReplyDelete