VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wanahitaji pongezi kwa kupambana kwa ajili ya uzi wa timu hiyo na kupata ushindi kwenye mchezo wa awali wa Kombe la Shirikisho.
Jana, Septemba 11, Azam FC ilipambana na kushinda katika mchezo wa awali kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Horseed FC.
Akizungumza na Saleh Jembe amesema kuwa wachezaji walipambana kwa hali na mali kusaka ushindi.
"Wachezaji wanastahili pongezi kwa kupambana kusaka ushindi ila bado kazi inaendelea na tunashukuru kwa ushindi," .
Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Septemba 18, Uwanja wa Uhuru na Horseed FC watakuwa wenyeji.
0 COMMENTS:
Post a Comment