September 2, 2021

 


TIMU ya Taifa ya Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen leo Septemba 2 imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya DR Congo.


Mchezo wa leo ambao ulikuwa ni wa kufuzu Kombe la Dunia dk 45 za mwanzo ngoma ilikuwa 1-1 na ni DR Congo walianza kumtungua Aishi Manula.


Bao la Tanzania lilifungwa na Simon Msuva dk 36 kwa shuti kali ambalo lilimshinda mlinda mlango wa DR Congo na kumfanya asawazishe bao la Merci Mbokane aliyepachika dk 25.


Nyota Msuva alikwama kuyeyusha dk zote 90 kwa kuwa alipata maumivu dk 89 na nafasi yake ilichukuliwa na Abraham Meshack. 


Pia katika mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa TP Mazembe nyota wawili wa Tanzania walionyeshwa kadi za njano ikiwa ni pamoja na Mzamiru Yassin na Feisal Salum hawa wote ni viungo wa kati.


Mchezo ujao wa Tanzania iliyo kundi J ni dhidi ya Madagascar unatarajiwa kuchezwa Septemba 7, Uwanja wa Mkapa.

3 COMMENTS:

  1. Mwanzo mzuri, waendelee kupambana

    ReplyDelete
  2. Hongera Sana stars. Watanzania tuna udhaifu mmoja ambao kama vile tunaona aibu kuuweka bayana kuwa ndio donda ndugu linalotutafuna kushindwa kufikia malengo na kupata mafanikio halisi tunayostahili, Udhaifu huo ni kushindwa kujiamini. Naamini kama Kim Pulsen angekuwa anafahamu kiswahili sawa sawa halafu akae chini ya vituo vya Radio na mitandao ya kijamii nakusikiliza jinsi wachambuzi wetu wa mpira walivyokuwa wakiiondoa kabisa Taifa Stars na kutarajia kupata kipigo cha aibu zidi ya Congo basi hata Kama Pulsen angeamua kuiacha Taifa Stars na kurudi kwao Denmark usingemlaumu.
    Msuva ni kiongozi mzuri anajiamini na kuwaaminisha wenzake kuwa hakuna kuogopa. Amepata ule ujasiri wa warabu. Uwepo ndani stars na mseto wa wachezaji kadhàa wenye uzoefu wa mashindano ya kiafrica kama wale wa simba watanzania tunatakiwa kuiamini Taifa Stars. Lengo hata kama si kufuzu lakini tunahitaji kupata matokeo kadhaa mazuri ili tuweze kupata mechi kadhaa kutupa uzoefu

    ReplyDelete
  3. madagasca watamkuta boko yupo fiti awatugue

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic