October 1, 2021


 KIWANGO alichokionesha kiungo mpya wa Yanga, raia wa Uganda, Khalid Aucho tangu atue hapo msimu huu, kimemtisha vilivyo kiungo wa timu hiyo, Mukoko Tonombe, kiasi cha kumlazimu kufanya mazoezi mara tatu kwa siku tofauti na ilivyokuwa awali

 Aucho ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga, alicheza kwa kiwango kikubwa mechi ya Ngao ya Jamii wikiendi iliyopita wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba. 

Katika mchezo huo, Mukoko alikosekana kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Spoti Xtra, limeelezwa kwamba, hasira za Mukoko kufanya mazoezi zaidi ya mara moja, zimetoka na kuhofia nafasi yake kuchukuliwa na Aucho.


“Kwa sasa Mukoko amelazimika kuongeza muda wa mazoezi yake, hii ni kwa sababu ya kukiona kiwango cha mrithi wake Aucho ambaye alifanya vizuri zaidi katika mchezo dhidi ya Simba.

“Mukoko amekuwa akipiga mazoezi asubuhi, mchana na jioni ambapo kuna program ya gym na ufukweni, kikubwa anataka kuhakikisha anaitetea namba yake kwani anafahamu akizembea tu, kocha atamuweka nje,” kilisema chanzo hicho.

Mukoko alikosekana pia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba ambapo Yanga ilishinda bao 1-0.

Mtupiaji alikuwa ni Feisal Salum ambaye alipachika bao hilo baada ya kipa wa Kagera Sugar, Chalamanda kupangua shuti la Fiston Mayele likakutana na mguu wa Fei Toto.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic