October 3, 2021


 KAIMU Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Yanga 
SC, Senzo Mbatha Mazingisa, amesema kuwa sasa wameanza kuiona Yanga ambayo walikuwa wakitamani kuiona kwa muda mrefu huku akisisitiza kuwa Wanayanga watarajie mambo makubwa msimu huu.


Yanga imefanikiwa kushinda mechi mbili za kwenye ligi ambapo ilianza kushinda bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera kisha jana ilishinda bao 1-0 dhidi ya Geita Gold.


Akizungumza na Championi Ijumaa, kiongozi huyo alisema kuwa licha ya ushindi walioupata dhidi ya Simba kwenye Ngao ya Jamii na katika ligi, ameweza kuona mabadiliko makubwa kwa Yanga kama timu kwa sababu hata wachezaji wamekuwa wakionyesha kiwango kizuri cha uchezaji tofauti na huko nyuma ambapo Yanga ilikuwa inacheza bila mpangilio.


“Ukitazama jinsi Yanga inavyocheza sasa dhidi ya timu pinzani utaona kabisa timu hii imekuwa na mabadiliko sana tofauti kabisa na michezo ya hapo awali ambapo tulipoteza kimataifa lakini naweza kusema kuwa hii ya sasa ndio Yanga ambayo tulikuwa tukitamani kuiona kama ambavyo inacheza sasa, kuna pasi unaziona zinapigwa wachezaji waonyesha uwezo wao kitimu na uwezo binafsi, ni mabadiliko makubwa kwetu.


“Binafsi naona kabisa tumepiga hatua kubwa,kuanzia tulivyocheza na Rivers United halafu tukacheza na Simba, naona kuna vitu vinaanza kubadilika, hivyo tuna imani kuwa msimu huu kuna mambo mazuri yanakuja kutoka kwa Yanga.


“Tulihitaji muda ili kuwa bora, hivyo tunashukuru ubora tunaanza kuuona, pongezi kwa benchi la ufundi, naona tumeanza na mwanzo mzuri,” alisema Senzo.

4 COMMENTS:

  1. Kbsaa baada ya mechi sita tutakaa sawa

    ReplyDelete
  2. Yanga hii kigoli kimoja tia maji tia maji hee👺

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba ilianza kwa kuifunga Biashara 3-0 kisha ikaifunga Dodoma Jiji goli 6-0 au sio??

      Delete
  3. Huyu jamaa hapa juu hajielewi kabisa,simba mna point ngapi na magoli mangapi? Pambanieni timu yenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic