SURE BOY AKIPOKEA TUZO KUTOKA KWA KATIBU MKUU TFF, ANGETILE OSIAH |
Nyota imezidi kung’aa kwa kiungo wa Simba, Amri Kiemba baada ya
juzi kufanikiwa kutangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
Kiemba alipata tuzo hiyo katika hafla fupi iliyofanyika juzi usiku
katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar. Hafla hiyo ya kutangaza washindi
wa tuzo mbalimbali za ligi kuu msimu uliopita, iliandaliwa na Chama cha
Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza).
Kiungo huyo aliwashinda nyota mbalimbali wakiwemo Haruna
Niyonzima, Didier Kavumbagu (Yanga), Kipre Tchetche (Azam FC) na Paul Nonga
(JKT Oljoro).
Tuzo ya kocha bora iliangukia kwa Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar ambapo
beki huyo wa zamani wa timu hiyo na kikosi cha Taifa Stars, aliwashinda Charles
Boniface Mkwasa (Ruvu Shooting), Abdallah Kibadeni (Kagera Sugar - sasa Simba)
na Jumanne Charles (Prisons).
KHATIM NAHEKA 'NTU WA NGUVU' WA CHAMPIONI NA MTU WANGU WA NGUVU MILLARD AYO WA CLOUDS FM WALIKUWA NDANI YA NYUMBA.. |
Nyota mwingine aliyeibuka kidedea ni kiungo wa Azam FC, Salum
Abubakar ‘Sure Boy’ aliyetwaa tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi akiwaacha Hassan
Dilunga (Ruvu Shooting), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Twaha Shekue (Coastal
Union) na Shomari Kapombe (Simba).
Pia kipa Hussein Sharif ‘Casillas’ (Mtibwa Sugar), alifanikiwa
kuwabwaga makipa wengine wawili katika tuzo ya kipa bora ambapo aliwashinda
Juma Kaseja (Simba) na Mwadin Ally (Azam FC).
0 COMMENTS:
Post a Comment