Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema hautamlipia
faini kocha wake wa makipa, Juma Pondamali ‘Mensah’.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kamati zake husika,
limempiga Pondamali faini ya Sh milioni moja na kumfungia kwa miezi mitatu
kutokana na kuonyesha vitendo visivyo vya kiungwana katika mechi dhidi ya
Yanga, hivi karibuni.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Ahmed Aurora, amesema timu hiyo haina
mpango wa kumlipia deni hilo.
“Yale ni mambo ya kujitakia, hivyo hatuna mpango wa kumlipia
deni hilo, sisi tutakachofanya hata kama tutamlipia hiyo lakini ajue ni lazima
tumkate kwenye mshahara wake,” alisema Aurora.
Siku hiyo, Pondamali alikwenda upande walipokuwa kuna
mashabiki wa Coastal ambao walikuwa wamekaa jukwaa lenye mashabiki wa Simba na
kuanza kucheza ngoma walizokuwa wakipiga.
Lakini wale wa Simba walianza kumzomea, naye akakasirika na
kuanza kuwaonyesha ‘vidole’.
0 COMMENTS:
Post a Comment