July 9, 2014



Beki na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amemwambia mshambuliaji anayetarajiwa kusajiliwa na Simba, Modo Kiongera kuwa msimu ujao atakuja na staili mpya ya ukabaji.


Kauli ya beki huyo imekuja baada ya kupata tetesi za Kiongera kutua Simba kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Cannavaro aliitaja staili ya ukabaji ameipa jina la ‘kugonga tu’ akiwa na lengo la kuzuia na kupunguza mashambulizi kwa washambuliaji wa timu pinzani.

“Kwenye msimu ujao wa ligi kuu, kiukweli sitakuwa na masihara kwa washambuliaji wa timu pinzani, nitarejea kivingine.

“Ninataka msimu ujao tuchukue ubingwa tuliopokonywa na Azam FC, hivyo sitakubali kuruhusu mabao golini kwetu, huyo mshambuliaji mpya wa Simba na hao wengine wa timu pinzani wajiandae kwa mapambano.

“Nitarejea kwa staili mpya ya ukabaji kwa washambuliaji wale wanaojifanya wasumbufu ambayo nimeipa jina la kugonga tu, hivyo washambuliaji wasubiri wataiona uwanjani,” alisema Cannavaro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic