Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga,
ameamua kuachana na klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita
aliokuwa akiutumikia klabuni hapo.
Kamwaga aliingia Simba akiwa katibu
mkuu wakati wa utawala wa mwenyekiti Ismail Aden Rage na sasa mkataba wake
umemalizika.
Kamwaga, awali alikuwa msemaji wa
klabu hiyo kabla ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa mwaka jana, ndipo Rage
akampandisha cheo na kuwa katibu mkuu.
Chanzo kutoka ndani ya Klabu ya Simba
kilieleza kuwa, katibu huyo amemaliza muda wake na haijajulikana kama
ataongezewa na uongozi mpya au la, lakini mwenyewe ametoa ufafanuzi na kudai kuwa
hataongeza.
“Kamwaga amemaliza mkataba wake
aliokuwa akiutumikia chini ya Rage na haijajulikana kama uongozi uliokupo
madarakani utamuongezea mkataba ama la,” kilisema chanzo hicho.
Kuhusiana na jambo hilo, Kamwaga ambaye kitaaluma ni mwanahabari alikiri kumaliza mkataba Simba:
“Nimemaliza mkataba wangu na sitaongeza
mkataba mwingine.”
0 COMMENTS:
Post a Comment