Uongozi wa klabu
ya Yanga chini ya Yusuf Manji umefanikisha zoezi ambalo litawawezesha wachezaji
wa kikosi cha Yanga kuwa na nyumba zao.
Wachezaji wa Yanga
pamoja na maofisa wa benchi la ufundi, watakopeshwa nyumba kupitia mishahara
yao.
Yanga imefanya
mazungumzo na Shirika la NSSF ambalo litawakopesha wachezaji hao nyumba zake
zilizo katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Taarifa zilizoifikia
SALEHJEMBE, zimeeleza Yanga pamoja na NSSF watafanya mkutano leo kutangaza
suala hilo.
Kutokana na hali
hiyo, wachezaji wa Yanga watakuwa wa kwanza kuingia kwenye rekodi ya kukopeshwa
nyumba.
Makato ya nyumba
hizo zinazoanzia Sh milioni 30 yatakuwa yanatokana na mishahara yao.







daaah vizuri sana
ReplyDeleteWashindwe wao tu wachezaji
ReplyDelete