Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani
Matola, amepewa mikoba ya kukinoa kikosi cha timu hiyo mpaka kocha mkuu,
Zdravko Logarusic, atakapowasili nchini keshokutwa alfajiri akitokea kwao, Croatia.
Simba inatarajiwa kuanza mazoezi kwa
ajili ya maandalizi ya msimu ujao kwenye Uwanja wa Ununio, huku asubuhi
ikitarajiwa kuanzia gym.
Uongozi wa Simba umesema taratibu zote za kuanza mazoezi
zimekamilika na kwamba leo asubuhi watakuwa wakianzia gym na jioni mazoezi ya
uwanjani wakiwa chini ya Matola.
Alisema wachezaji wote wa kimataifa na
wapya waliosajiliwa wameshapewa taarifa za kuanza kwa mazoezi na kwamba leo
watakuwepo uwanjani isipokuwa Donald Musoti anayetarajiwa kuwasili leo Jumatano
akitokea Kenya.
“Kocha Loga atakuja Alhamisi, lakini
Musoti yeye atakuja kesho (leo), wachezaji wengine wote tumeshawataarifu juu ya
kuanza mazoezi,” alisema Msemaji wa Simba, Muhaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment