July 11, 2014



Uongozi wa timu ya Fanja ya Oman, pamoja na kocha wao wa zamani, Talib Hilal, umewatumia Simba salamu za pongezi baada ya kufanikiwa kufanya uchaguzi wa viongozi wapya.


Simba ilifanya uchaguzi mkuu siku chache zilizopita, huku Evans Aveva akifanikiwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi jijini Dar.

Fanja wamekuwa na uhusiano mzuri na Simba kwa muda mrefu na msimu uliopita waliialika timu hiyo kwenda Oman kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya msimu.

Katika barua hiyo ambayo SALEHJEMBE INA NAKALA YAKE, Fanja wamesema wanafurahia kuona timu hiyo imefanya uchaguzi huo kwa amani na wanafurahia kwa kuwa wataendeleza uhusiano wao mzuri na viongozi wapya wa Msimbazi.

“Fanya imekuwa na uhusiano mzuri sana na Simba kwa muda mrefu, uhusiano huu umekuwa ukiboreshwa zaidi na mchezaji wao wa zamani na nahodha Talib Hilal.

“Talib bado amekuwa na uhusiano wa karibu sana nasi, tunaamini kuwa uongozi mpya utaendeleza uhusiano ule wa awali,” ilisema barua hiyo.

Uchaguzi wa Simba uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita, mbali na Aveva lakini viongozi wengine ni Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye alichaguliwa kuwa makamu wake na wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic