MBEYA CITY |
Klabu ya Mbeya City,
imetamba kuhakikisha inaendelea kupata ushindi katika mchezo wao ujao dhidi ya
Tanzania Prisons.
Mbeya na Prisons zitavaana
Jumamosi wiki hii katika mechi ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na
upinzani wa timu zote mbili.
Mbeya City kwa sasa ina
alama 11 baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar wikiendi
iliyopita na kwa sasa ipo katika nafasi ya 11, ingawa mwendo wa timu hiyo
umeonekana kusuasua tofauti na msimu uliopita.
Ofisa habari
wa timu hiyo, Dismas Ten, alisema
maandalizi yao yanakwenda vyema na lengo lao ni kuhakikisha wanaondoka na
ushindi licha ya ligi kuonekana kuwa ngumu.
“Tumejipanga vyema, ni mechi ngumu lakini tutapambana ili kuweza
kuibuka na ushindi ili kuwa katika nafasi nzuri zaidi japo ni mchezo mgumu na
wote tunakuwa katika uwanja wa nyumbani.
“Na kama mnanyofahamu
Prisons kwa sasa siyo wa kubeza, ni timu nzuri sana, hivyo tunatakiwa kuwa
makini sana,” alisema Ten.
0 COMMENTS:
Post a Comment