March 10, 2015


Kiungo nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima ameshangazwa na taarifa kwamba yeye amefukuzwa kambini.


Niyonzima amesema taarifa zilizokuwa zikisikika kuanzia saa 10 jioni leo ni uzushi mtupu.

"Nimesikia, pia watu wengi wamenipigia kuniuliza. Ukweli ni kwamba hakuna ukweli katika hilo na mimi nilikuwa nje ya kambi kwa ruhusa maalum.

"Nafikiri watu wanataka kutengeneza maneno na kutuletea uchonganishi tu," alisema Niyonzima.

Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Yanga, Jerry Muro yeye alisema taarifa za Niyonzimana Danny Mrwanda kufukuzwa, hazina ukweli.

"Ni maneno yasiyo na ukweli na hakuna mchezaji aliyefukuzwa kama inavyoelezwa," alisema Muro.

Niyonzima alilambwa kadi nyekundu katika mechi iliyopita wakati Yanga ilipolala kwa bao 1-0 dhidi ya Simba, Jumapili.


1 COMMENTS:

  1. Tatizo yanga viongozi wao wanashindwa kuwaandaa wachezaji kisaikolojia badala yake wanabaki kuongea na vyombo vya habari tu hilo ni tatizo kubwa sana litawatesa yanga mda mrefu kila wakikutana na simba ni kipigo tu mimi kama mjumbe wa kamati ya mashindano uwa tunaongea na mchezaji mmoja mmoja tunamwanda kisaikorojia ndio maana tunawafunga yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic