Klabu ya Simba, imetoa ruhusa kwa timu zinazotaka kuwasajili wachezaji kutoka katika kikosi chake kujitokeza na kuzungumza nao.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kamwe hawawezi kuwazuia wachezaji wao kama wanataka kuondoka.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Hans Poppe amesema wachezaji ambao mikataba yao imefikia ukingoni, tayari wameanza mazungumzo nao.
"Lakini kama mtu atataka kuondoka, hatuwezi kumzuia. Timu ambayo inamtaka, basi inaweza kuzungumza naye.
"Kwetu tumeishaanza mazungumzo nao. Mtu anayetaka kubaki kufanya kazi nasi, pia tunazungumza naye. Si kumlazimisha ambalo haliwezi kuwa jambo sahihi," alisisitiza Hans Poppe.
Baadhi ya nyota wa Simba, mikataba yao imefikia ukingoni hali ambayo imekuwa ikiwapa hofu mashabiki wa Msimbazi wakidhani huenda watawakimbia.
0 COMMENTS:
Post a Comment