CHANONGO (NAMBA 8) AKISHANGILIA NA WACHEZAJI WENZAKE WA STAND UNITED AMBAYO ANAITUMIKIA KWA MKOPO. |
Klabu
ya Simba SC inatakiwa kumlipa mchezaji Haruni Chanongo Sh 11,400,000,
kufikia leo! Vinginevyo Sekretarieti ya TFF itaanza kukata mapato ya
Simba ili kumlipa mchezaji huyo.
Iwapo
Simba itakuwa na vielelezo vingine katika kikao kinachofuata cha Kamati
kitakachofanyika Mei 3, 2015 itafanywa hesabu na Simba kurejeshewa fedha
itakayokuwa imezidi.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imeagiza kwa klabu ya Simba na klabu
nyingine zote kuwa kwa wachezaji wa mkopo, maslahi yao (mishahara na posho)
yote yailipwe na klabu husika kwa klabu ambayo mchezaji anakwenda kwa mkopo ili
malipo yake yawe yanafanyika kutoka kwenye klabu moja badala ya kufuatilia
malipo yake katika klabu mbili tofauti, hali hii inaweza msabababishia usumbufu
mchezaji aliye kwenye mkopo.
0 COMMENTS:
Post a Comment