Kamati ya
Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF limetangaza Uchaguzi Mkuu
wa klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga utafanyika tarehe 05, Julai 2015.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Melchesedek Lutema ametoa ratiba ya
mchakato mzima wa uchaguzi huo, ambapo tarehe 21-22 Mei mwaka huu zitatangazwa
nafasi zote zinazogombewa.
Kwa mujibu
wa kalenda hiyo ya Uchaguzi, tarehe 23-30, Mei 2015 itakua ni kipindi cha
uchukuaji fomu kwa wagombea wote na kuzirudisha, wakati Juni Mosi mpaka Juni
04, 2015 ni kipindi cha mchujo wa awali kwa wagombea.
Juni 05,
2015 Kamati ya Uchaguzi itatoa orodha ya awali ya wagombea, Juni 7-9, 2015
itakua ni kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea, na Juni 10-11
ni kupitia mapingamizi yote.
Julai 02
-04, 2015 ni muda wa kampeni kwa wagombea wote na uchaguzi mkuu utafanyika
tarehe 05, Julai 2015.
Ratiba
kamili ya mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Coastal Union imeambatanishwa
0 COMMENTS:
Post a Comment