Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo inashuka dimbani kucheza mchezo wake wa
pili dhidi ya timu ya Taifa kutoka Madagascar, mchezo utakaochezwa katika
uwanja wa Royal Bafokeng majira ya saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Taifa
Stars inahitaji kupata ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Madagascar ili
kufufua matumaini ya kuweza kusonga mbele katika hatua inayofua ya Robo
Fainali.
Kocha Mkuu
wa Taifa Stars akiongelea mchezo wa leo amesema, makosa yaliyojitokeza katika
mchezo dhidi ya Swaziland yamefanyiwa kazi na anaamini vijana wake watafanya
vizuri.
“Mchezo wa
Swaziland tulipata nafasi nzuri za kufunga, lakini washambuliaji wangu hawakuwa
makini kuzitumia nafasi hizo, tatizo la kupoteza nafasi nyingi limefanyiwa kazi
na nina amini leo vijana watafanya vizuri” alisema Nooij.
Aidha
Nooij amesema anataarajia mchezo kuwa mgumu kutokana na Madagascar kuhitaji
ushindi wa pili mfululizo, baada ya kuifunga Lesotho katika mchezo wa awali,
Nooij ameahidi kufanya vizuri katika mchezo huo.
Mchezo huo
utakuwa moja kwa moja (Live) katika kituo cha Superspot SS4, na SS9.
Naye
kiungo wa Taifa Stars, Said Juma Makapu anarejea nyumbani leo usiku kwa usafiri
wa Shirika la ndege la Fastjet kwa ajili ya kufanyia vipimo zaidi na matibabu,
anatarajiwa kuondoka uwanja wa O.R. Tambo saa 5 usiku kufika uwanja wa JK
Nyerer saa 8 usiku.
0 COMMENTS:
Post a Comment