NIANG |
Kocha wa viungo wa Simba, Mserbia, Dusan
Momcilovic, amefichua kuwa straika Msenegali, Papa Niang alidanganya kuwa yupo
fiti wakati hakuwa fiti na hiyo ilichangia ashindwe katika majaribio ya
kuichezea timu hiyo.
Momcilovic amesema baada ya Niang kutua klabuni
hapo, alimuuliza kama yuko fiti ambapo mchezaji huyo alisema yupo fiti lakini
haikuwa hivyo kwani hakuwa fiti.
“Niang alipokuja nilimuuliza kama yupo fiti
akasema ndiyo na kudai siku tatu tu nyuma alitoka kucheza mechi na timu yake ya
taifa, nilipompima nikagundua siyo kweli, hakuwa fiti, baadaye nikamuuliza kama
anaweza kucheza, akasema ndiyo, alipopangwa ndiyo hivyo tena. Alihitaji zaidi
ya siku 45 kuwa fiti kabisa,” alisema Momcilovic.
Aidha, taarifa nyingine zinadai straika huyo
hakuwa amecheza kwa muda mrefu kabla ya kuja nchini, ndiyo maana katika mechi
ya Mwadui FC alichemka.
0 COMMENTS:
Post a Comment