LIBYA |
Na Saleh Ally, Kartepe
Taifa Stars inatarajiwa kushuka dimbani leo Ijumaa kucheza mechi ya mazoezi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Libya ambayo pia imeweka kambi katika mji huu wa Kartepe, Uturuki.
Taifa Stars inatarajiwa kushuka dimbani leo Ijumaa kucheza mechi ya mazoezi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Libya ambayo pia imeweka kambi katika mji huu wa Kartepe, Uturuki.
Taarifa
zilizotoka jana usiku, mechi hiyo itapigwa saa 5 asubuhi kwa saa hapa pia
nyumbani Tanzania
Libya inanolewa na kocha maarufu na mkongwe
duniani, Javier Clemente, raia wa Hispania, ambaye amewahi kuzifundisha klabu
maarufu na timu mbalimbali za taifa.
Clemente ,65, raia wa Hispania, aliyewahi kuzinoa
klabu za Athletic Bilbao, Atletico Madrid, Real Betis, Real Sociedad, Espanyol
na Tenerife, amesema ana imani Stars itampa ushindani.
Clemente amesema amefurahishwa kuona Stars ina
wachezaji wengi vijana.
“Nilipita tu kwenye mazoezi yao, inaonekana wana
wachezaji wengi sana vijana. Ndiyo maana nakuambia nategemea upinzani wa juu.
“Najua Ijumaa kutakuwa na mechi nzuri ya mazoezi
na hilo ndilo hasa lengo la kuwa hapa. Kufanya maandalizi bora,” alisema Clemente
ambaye pia amewahi kuzinoa timu za taifa za Serbia, Cameroon kabla ya kutua
Libya.
Kocha huyo amefundisha zaidi ya timu 10 za
Hispania katika La Liga, pia amewahi kuinoa Marseille ya Ufaransa, moja ya timu
kubwa nchini humo. Licha ya nchi yake kuwa na vita, Libya imekuwa ukihakikisha
timu yake ya soka inazidi kuwa imara.
0 COMMENTS:
Post a Comment