October 11, 2015


Mgombea wa Udiwani Mbagala Kuu kupitia CCM, Yusuf Manji leo amefanya mkutano unaoweza kuitwa mafuriko kutokana na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi.

Mkutano huo uliofanyika Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam, Manji alipokelewa kwa shangwe wakati akiingia huku akiongozana na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu na viongozi wengine wa CCM pamoja na wagombea wote wa udiwani wa CCM jijini Dar es Salaam.

Wasanii kadhaa wa Bongo Fleva wakiwemo Tunda Man, Dogo Janja, Chid Benz na wengine walipata nafasi ya kutumbuiza.

Baada ya hapo, Manji alipata nafasi ya kuhutubia na mara nyingi wananchi walikuwa wakimshangilia kwa nguvu kuonyesha wanaunga mkono anachokizungumza.

Idadi kubwa ya watu waliojitokeza ndiyo ilikuwa gumzo huku ikilinganishwa na wagombea kadhaa wa Urais huku ikionekana baadhi ya wagombea wa urais hawakuwahi kupata idadi kubwa ya watu kama hiyo.

CHEKI PICHA ZAIDI....





 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic