January 21, 2016


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kamwe hawatafanya mzaha katika mechi yao ya leo dhidi ya Majimaji ya Songea.

Yanga inaivaa Majimaji iliyo katika hatari ya kuteremka daraja katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

Yanga itakuwa inapambana kuhakikisha inapata pointi tatu ili ifikishe pointi 39 sawa na Azam FC na kurejea kileleni kwa tofauti ya mabao.

Katika mechi yake ya mwisho kwenye Uwanja huo, Yanga ilifanya kazi ya ziada kuhakikisha inapata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC iliyoonekana kuwa ngumu kinoma.

“Mechi za Ligi Kuu Bara zinakwenda zinabadilika, zinazidi ugumu kwa kuwa kila timu inazidi kuongeza umakini. Kila timu inapambana kubaki kwenye ligi na kama unaona Majimaji wako katika wakati mgumu,” alisema Pluijm.

“Tutajitahidi kucheza vizuri na ikiwezekana kuumaliza mchezo mapema ili kujiweka katika hali nzuri ya kuondoa presha baadaye,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic