January 21, 2016

TAMBWE (MBELE) NA NGOMA

Kweli sasa Yanga hawataki “utani na kazi” baada ya leo kurejea kileleni kwa kushinda kwa kuitwanga Majimaji ya Songea kwa mabao 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wakati Yanga ikirejea kileleni kwa idadi kubwa ya mabao ya kufunga na machache ya kufungwa, mshambuliaji wake Amissi Tambwe, amepiga hat trick.

Tambwe raia wa Burundi amefunga mabao matatu huku mawili yakifungwa na Wazimbabwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoko aliyefunga la kwanza.

Kamusoko alifunga bao la kwanza lililodumu hadi mapumziko na baadaye Yanga ikacharuka kipindi cha pili na kuwatandika vijana wa Kalimangonga Ongalla aliyewahi kuichezwa Yanga.


Deus Kaseke leo alikuwa mwiba kwa mabeki wa Majimaji akishirikiana na beki wa kulia, Juma Abdul.

1 COMMENTS:

  1. Kweli hawa watani wangu Yanga wanajua aiseeee,napenda walivyo na ushirikiano,hakuna uchoyo kwenye kutoa pasi zao,na kwa jinsi hiyo
    wanachokitaka pia mfungaji bora atoke kwao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic