March 15, 2016

KABURU

Uongozi wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam umesema umefika mbali katika suala lake na beki wake, Hassan Kessy na una imani kubwa ataendelea kubaki na kuitumikia klabu hiyo msimu ujao.

Makamu Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema wameanza mazungumzo na Kessy na yako katika hatua nzuri sana.

“Tuko katika hatua nzuri sana ya mazungumzo. Tumeanza mazungumzo kipindi sasa na tuna matumaini makubwa Kessy ataendelea kubaki Simba,” alisema Kaburu katika mahojiano na SALEHJEMBE.

KESSY

“Tunaamini Kessy tunamhitaji, naye ni kijana anayeipenda Simba. Hivyo tukifikia makubaliano, tutaingia mkataba na kuwataarifu.”

Kumekuwa na taarifa huenda Kessy ana mpango wa kujiunga na Yanga hali iliyoonyesha kuwaudhi baadhi ya mashabiki wa Simba.


Hata hivyo kumekuwa na mgawanyiko kuhusiana na beki huyo wa kulia mwenye uwezo wa kupiga krosi nyingi. Wengine wakisema abaki na wengine wakikubali aende zake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic