Ili kuhakikisha wanavuna pointi tatu mechi dhidi ya Azam FC ili waendelee kubaki kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, mabosi wa Yanga wamekamilisha ahadi yao waliyoitoa kwa wachezaji ya kuwapa shilingi milioni 15.
Mabosi hao wa timu hiyo, waliitoa ahadi hiyo ya fedha kama watafanikiwa kuwafunga wapinzani wao Simba katika mechi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo Yanga ilishinda kwa mabao 2-0, hivyo uongozi umeamua kutimiza ahadi kwa vitendo.
Taarifa ambazo Championi Ijumaa limezipata kutoka ndani ya Yanga ni kuwa, fedha hizo ni kama motisha ili Azam wale kichapo kesho Jumamosi.
Alipotafutwa Mkuu wa Idara wa Habari na Mawasiliano ya timu hiyo, Jerry Muro kuzungumzia hilo alisema: “Hatutaki kuongea chochote hivi sasa, hivi sasa akili yetu imeelekezwa kwenye mchezo wetu na Azam ili tuendelee kubaki kileleni.”
0 COMMENTS:
Post a Comment