KINYOGOLI AKIWA MAZOEZINI YANGA |
Askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Makao Makuu Dar es salaam, Sajini Kinyogori ameuawa usiku wa kuamkia leo kupigwa risasi nyumbani kwake eneo la Mwandege, Mkuranga Pwani.
Kinyogoli alikuwa alikuwa shabiki mkubwa wa Yanga, mara nyingi alijitokeza mazoezini na picha zake nyingi alikuwa akivaa jezi za Yanga.
Pia alikuwa maarufu kutokana na kusikika mara kwa mara kwenye kipindi cha asubuhi cha Radio One cha "Usalama Barabarani."
Watu waliompiga risasi hawajajulikana na imeelezwa walikwenda nyumbani kwake usikus aa tatu na kufanya shambulizi hilo.
"Walifika pale na kugonga, walitoka watoto kufungua wakawaambia wawaitie baba. Kweli walikwenda kumuita, alipotoka tu wakamshambulia kwa risasi tatu, mbavuni, mkononi na kichwani," alisema shuhuda.
"Tayari mwili wake tumeuhifadhi Muhimbili na linalofuatia ni suala la ndugu, kweli inasikitisha sana jamani."
0 COMMENTS:
Post a Comment