June 24, 2016

IBRAHIM (KUSHOTO) AKIWA NA RAIS WA SIMBA, EVANS AVEVA WAKATI WA KUSAINI MKATABA WA KUJIUNGA NA TIMU HIYO.

Kiungo mpya wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘Rasta’ ameonyesha kweli amepania kufanya kweli  na kupata nafasi katika kikosi cha kwanza, hii ni kutokana na kutumia saa tatu akifanya mazoezi makali juani.

Ujio wa kiungo huyo unaonyesha ni kama kutaka kumpiku Mwinyi Kazimoto, ambaye alikuwa akipata nafasi kwenye kikosi cha kwanza muda mwingi msimu uliopita akipokezana na Said Ndemla.

Ujio wa Rasta aliyetokea Mtibwa Sugar kwa kitita cha shilingi milioni 30, utaongeza changamoto.

 Rasta kwa sasa yupo bize na mazoezi kwenye Uwanja wa Garden uliopo Vijana-Kinondoni, akiwa na wachezaji wengine wa timu hiyo na timu tofauti.

Baadhi yao ni Danny Lyanga, Peter Manyika na Said Ndemla (Simba), Mohammed Mkopi (Prisons), Rashid Mandawa (Mwadui), William Lucian ‘Gallas’ na Aziz Sibo (Ndanda).

Kuhusiana na maandalizi hayo Rasta amesema: “Tukitoka hapa, kuna program zangu binafsi nazifanyia nyumbani, gym ninatarajia kuanza rasmi wiki ijayo.

“Kikubwa ujue Simba ni timu kubwa, ina wachezaji wenye viwango vyao, hivyo lazima ujiweke fiti kwa ajili ya kukabiliana na upinzani wa namba,” alisema Rasta.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV