June 24, 2016


Huku homa ya pambano la vigogo Yanga na TP Mazembe ikizidi kupanda, kikosi cha TP Mazembe kinatarajiwa kutua Dar es Salaam, keshokutwa Jumapili, ikiwa siku mbili kabla ya mchezo wenyewe wa hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema Mazembe wanatarajiwa kufikia katika Hoteli ya Serena, moja ya hoteli chache za kifahari zenye nyota tano jijini Dar es Salaam.

“Mpaka sasa taarifa tulizonazo kutoka kwao ni kwamba watafika Jumapili na watafikia Hoteli ya Serena. Hizo ndizo taarifa walizotupa kwa sasa, kuhusu msafara wao utakuwa na jumla ya watu 32,” alisema Lucas.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV