July 7, 2016

 Kipa Aishi Manula wa Azam FC amepata mpinzani kwa kuwa kipa Daniel Yeboah Tetchi raia wa Ivory Coast ametua nchini jana.

TAarifa za uhakika zinasema Tetchi amekuja kusaini tu na si vinginevyo ingawa kuna kipa kutokea Tenerife ya Hispania ambaye pia anahitaji kujiunga na Azam FC. Maana yake lazima wapewe nafasi ya kuonyesha ujuzi na nani achukue nafasi hiyo.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 31, alianza kuonyesha cheche zake akiwa Asec Mimosa ya Ivory Coast.
Pia amewahi kuitumikia Dijon ya Ufaransa katika kikosi chake cha pili.


Habari za uhakika zinaeleza, Tetchi yuko katika nafasi kubwa ya kumalizana na Azam FC lakini suala la kipa Mhispania linaweza kuweka ushindani mbele yake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV