October 21, 2016Hatma ya vurugu zilizotokea kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza kati ya Coastal Union na KMC uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga itajulikana leo baada ya Kamati ya Saa 72 kuketi kujadili ripoti za mchezo huo.

Hata hivyo kumekuwa na hofu kwamba, huenda Coastal Union inaweza kuondolewa kwenye uwanja huo kutokana na tabia za mashabiki wake kuwapiga waamuzi mara kwa mara.

Mchezo huo uliopigwa Jumapili iliyopita ulimalizika kwa vurugu kali kwa mwamuzi wa kati, Thomas Mkombozi kushambuliwa kwa mawe na silaha nyingine na mashabiki waliodhaniwa kuwa wa Coastal Union, waliomtuhumu ‘kuinyonga’ timu yao iliyochezea kichapo cha mabao 3-2.


Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, amesema pamoja na kusubiria maamuzi ya kamati hiyo, kanuni za wazi ni kwamba iwapo ripoti zitabainisha mashabiki ndio wenye makosa, basi Coastal kuna hatari ya kucheza mechi zilizobaki bila mashabiki ama kuhamishwa kutoka uwanjani hapo.

Mashabiki wa Coastal Union wamekuwa wakikumbana na shutuma ya kuwapiga waamuzi wa soka kwa madai ya kuwa wanaibana timu yao kwa makusudi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV