February 12, 2017


Mshambuliaji Laudit Mavugo wa Simba, ndiye amekuwa gumzo zaidi katika mijadala mbalimbali baada ya kufunga mabao katika mechi mbili mfululizo.

Mavugo amefunga katika mechi dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana. Lakini kabla alikuwa amefunga dhidi ya Majimaji.

Mbali na hivyo, raia huyo wa Burundi, alitoa pasi ya bao la Ibrahim Ajibu na katika mechi zote mbili Simba imeshinda kwa idadi sawa ya mabao matatu.

Katika mijadala inayoendeshwa mitandaoni na mashabiki wa soka, wengi wanaamini Mavugo ameanza kuimarika na kuizoea ligi ya Tanzania.


Wako ambao wanaamini wengine walikuwa na haraka dhidi ya mshambuliaji huyo ambaye hapendi purukushani lakini ni hatari anapokuwa na mpira.

Lakini wako wanaoamini, Kocha Joseph Omog hakuwa akimpa nafasi ya kutosha ili Mavugo aizoee Ligi Kuu Bara ambayo ina purukushani zaidi ya ile ya kwao Burundi au Rwanda alipowahi kucheza.

4 COMMENTS:

  1. Mnyama jana kupiga mpira mwingi sana na safu ya ushambuliaji ambayo siku za nyuma tuliona imepotea jana ilikuwa tishio hasa muunganiko wa ajibu mavugo na liuzio ambao walionana vizuri na kuichachafya ngome ya prison..Hata walipoingia kina kichuya na pastory walionyesha soka safi la kupambana tofauti na siku za nyuma ambazo pastory alionekana kwa ulegevu na kuchezewa faulo nyingi ambazo hazikuwa na faida kwetu..ukimwangalia kichuya jana alifanya vitu kama vya mwanzo wa msimu ambapo aliweza kusogea Langoni na kugongesha besela kwa shuti Kali..kimsingi simba ikicheza hivi mechi zilizosalia ndoo yetu hiyo haina ubishi kwani kwa mpira wa jana hata yeboyebo wangekaa...Viva Simba sports club

    ReplyDelete
  2. Cha msingi ni kuzudi kumuamini kila mchezaji kwan huwez ukafanya vzr kwa mara moja smtyms mpira unaitaji muda...

    ReplyDelete
  3. Safi mwendo huu huu hadi mwisho

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic