May 29, 2017Pamoja na taarifa za kiungo Ibrahim Ajibu kuelezwa amejiunga na Singida United, yeye amesisitiza bado ni mchezaji wa Simba.

Ajibu amesema mkataba wake unaisha mwezi ujao lakini kikubwa bado ni mchezaji wa Simba.

“Hadi uone nimesaini au nakabidhiwa jezi basi unaweza kusema kweli.


“Lakini kwa sasa naacha kila mmoja aseme anavyoamini, lakini mimi ni mchezaji wa Simba,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV