July 20, 2017




Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limewateua waamuzi wa Uganda kuchezesha mchezo wa marudiano kati ya Amavubi ya Rwanda na Taifa Stars ya Tanzania. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Nyamirambo, Jumamosi saa 10.00 jioni kwa saa za Rwanda sawa na saa 9.00 alasiri kwa saa za Tanzania, utachezeshwa na Brian Nsubuga Miiro ambaye atakuwa na jukumu la kupiliza kipenga.

Waamuzi wasaidizi watakuwa Ronald Katenya (Line 1) na Dick Okello (Line 2) wakati Mwamuzi wa akiba atakuwa Chelanget Ali Sabila huku Kamishna wa mchezo atakuwa Ali Mohamed Ahmed kutoka Somalia.


Mchezo huo ni wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN). Timu hiyo kwa mwaka huu imecheza mechi 10 za kimataifa na kushinda mitano; kutoka sare minne na kufungwa mmoja wa nusu fainali za Cosafa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic