August 10, 2017Haruna Niyonzima ameishamalizana na Simba na kuanza kazi, lakini haikuwa kazi rahisi kwa viongozi wa Simba wanaohusika na usajili.

Siku anaanza mazoezi ikiwa ni siku moja kabla ya tamasha la Simba Day, baadhi ya vigogo wa Simba akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe walilazimika kufika mazoezini.

Hans Poppe akiongozana ana kigogo mwingine, Mohamed Kigoma walikuwa mazoezini pale wakipiga 'chabo' wakati Niyonzima akiingia mazoezini.

Walionekana wazi walitaka kuhakikisha kweli ameanza mazoezi na si hadithi tena.

Walikuwa wakiangalia kwa umakini mkubwa wakati akifika hadi anaingia na wakakaa kuhakikisha wanamaliza mazoezi na kila kitu kinaenda sawa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV