August 10, 2017


Siku Haruna Niyonzima alipoanza mazoezi, baadhi ya mashabiki wa Simba walikuwa kama wendawazimu, maana hawakuamini.

Yeye alikuwa ndani ya gari lililoegeshwa karibu kabisa na eneo la Uwanja wa Boko Veterani. Baada ya mashabiki hao kujua walivamia sehemu ilipo gari hiyo na kuanza kumtafuta kama kweli yumo.

Walipopata uhakika, mashabiki hao wakaanza kulisukuma gari hilo wakimtaka dereva wala asisimbuke.

Hiyo ilikuwa ni uamuzi wa mashabiki hao kutumiza furaha yao. Tayari Niyonzima ameanza kuichezea Simba katika mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports na Simba ikaibuka na ushindi wa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV